
Fursa ya maridhiano ya kisiasa nchini Tanzania baada ya hukumu ya Tundu Lissu
Novemba tarehe 6, Mahakama Kuu jijini Dar es salaam nchini Tanzania, ilimhukumu miaka minne jela Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kosa la uchochezi, baada ya kumwondolea kesi ya uhaini aliyokuwa ameshtakiwa nayo na kuzuiwa gerezani tangu alipokamatwa Aprili 9, 2025. Tundu Lissu na chama chake, wanasema hukumu hiyo ni ya kisiasa. Kuna uwezekano wa maridhiano ya kisiasa nchini Tanzania? Tunachambua na mtaalam wa siasa na utatuzi wa migogoro Francis Ibrahim.
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

