
Hatima ya serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar
Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, amezindua Kamati ya pamoja ya majadiliano kati ya chama chake CCM na kile cha upinzani ACT Wazalendo, katika kile kinachoashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa katika visiwa hivyo. Hatua hii inakuja baada ya vyama hivyo kusaini tamko la pamoja la makubaliano Julai tarehe 9 mwaka huu, ili kupata maridhiano ya kisiasa. Kwanini imechukua muda mrefu kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar? Tunachambua.
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

