
Kwa nini afya ya akili ni swala muhimu kwa wagonjwa wanaougua magonjwa sugu
Shirika la afya duniani ,WHO limesema watu zaidi ya milioni 150 barani Afrika wana hitaji huduma za afya ya akili. Kutokana na idadi hii inayopanda kila wakati ,watalaam wa afya wanasisitiza wagonjwa walio kwenye matibabu ya magonjwa yasiyoambukizwa sharti kufuatiliwa pia kwa matatizo ya afya ya akili ,chini ya mpango wa huduma za afya jumuishi. Wataalam wanasema matibabu ,gharama kubwa na mabadiliko ya haraka yanayoambatana na magonjwa haya yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha matatizo ya afya ya akili kwa mgonjwa Dawa zinazotumika pia zinaweza kuwa chanzo cha matatizo kama msongo wa mawazo,sonona na kiwewe miongoni mwa wagonjwa hao.
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

