
Maji ya barafu na kutembea bila viatu inavyotibu mishipa na sonona
Watu wengi wameanza kukumbatia matibabu yasiyo ya dawa kuyatibu baadhi ya matatizo ya kiafya. Miongoni mwa matatizo hayo ni matatizo ya mishipa,viungo na matatizo ya afya ya akili Dkt Hamisi Kote Ali ni mmoja wa madaktari ambao wanatoa matibabu hayo ambayo yanafahamika kama matibabu ya 'Chiropractic'. Katika makala haya Dkt Hamisi anaelezea faida za kutembea bila viatu ambapo anatumia mfano wake ,akiwa hajavalia viatu kwa miaka saba sasa. Aidha anafafanua kuhusu zoezi la kutumbukizwa na kukaa ndani ya maji ya barafu linavyofanya kazi na baadhi ya matatizo yanayoweza kutibika kwa njia hiyo.
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.
