
Kifafa cha mimba bado kinasababisha vifo vingi vya akina mama na watoto Afrika
Kifafa cha mimba hali inayohusishwa na shinikizo kubwa la damu mama anapokuwa mja mzito kuanzia wiki 20 za mimba na inaweza kujitokeza pia pindi mama anapojifungua ,ni hali ya dharura na tishio kubwa kwa akina mama waja wazito Watalaam wanahoji kuwa hatari yake hutokana na kwamba dalili zake wakati mwingi hufanana na dalili za kawaida za mama mja mzito Ni kutokana na hili mashirika ya kijamii kutoka mataifa matano ya Afrika yanashinikiza uwekezaji kwenye kubainisha ,kuzuia na kutoa huduma kwa akina mama waja wazito. Isitoshe ushirika kwa wanaume kwenye maswala ya uzazi ili wanapokuwa wana ufahamu wanaweza kusaidia kwenye mapambano hayo
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

