
Wagonjwa wa saratani wanavyochanganya matibabu ya hospitali na mazoezi
Wagonjwa wengi wa saratani mara nyingi huhisi kulemewa na madhara yanayotokana na matibabu makali ambayo wanabidi kutumia kwa muda mrefu. Kurahisisha safari hiyo kituo cha Faraja Cancer Support Trust eneo la Parklands Nairobi kimewapa fursa ya kufanya mazoezi; na kucheza muziki huku wakiendelea na matibabu hayo. Wengi ambao wamekuwa wakishiriki mazoezi hayo wanasema miili yao ina uimara zaidi, wana ari mpya kupambana na wanaongeza furaha katika maisha yao kutokana na kupata marafiki ambao wanahimizana namna ya kuushinda ugonjwa wa Saratani.
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.
