Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

“Usugu dhidi ya viuavijasumu AMR hauonekani, lakini mimi ninaonekana” - Manusura John Kariuki
Usugu dhidi ya viuavijasumu (AMR) au antibiotiki ni tishio lisiloonekana kwa macho, lakini madhara yake yanaweza kugharimu maisha. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO) linaonya kuhusu hatari hii inayofanya maambukizi kuwa magumu, na wakati mwingine kushindikana kabisa kutibika. Kwa John Kariuki, kutoka Kenya manusura wa AMR, hatari hii si hadithi tu ni hali halisi kwani maambukizi aliyopata baada ya kufanyiwa upasuaji yalimweka kwenye hatari ya kupoteza maisha, baada ya dawa 17 kati ya 18 za viuavijasumu zilizojaribiwa kushindwa kukabiliana na maambukizi hayo. Ni nini hasa kilimtokea, na ana ujumbe gani kwa dunia katika wiki hii ya kuamasisha kuhusu usugu wa viuavijasumu? Ungana na Flora Nducha katika simulizi hii.
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

