Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunaangazia simulizi ya manusura ya Usugu dhidi ya viuavijasumu (AMR) nchini Kenya, mauaji ya kimbari ya waRohingya nchini Myanmar, na kilim ona ufugaji endelevu inayohimili mabadiliko ya tabianchi nchini Zimbabwe.
• Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki, (ICJ) imesema kuwa Myanmar ilifanya mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya wachache ya Warohingya jimboni Rakhine. Uamuzi huo, umetolewa leo huko The Hague na jopo la majaji 15 kutoka mataifa mbalimbali duniani, ikiwa ni kesi ya kwanza katika historia ambapo taifa linapatikana na hatia na Mahakama ya Kimataifa ya kutekeleza mauaji ya kimbari
• Usugu dhidi ya viuavijasumu (AMR) au antibiotiki ni tishio lisiloonekana kwa macho, lakini madhara yake yanaweza kugharimu maisha. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO) linaonya kuhusu hatari hii inayofanya maambukizi kuwa magumu, na wakati mwingine kushindikana kabisa kutibika. Kwa John Kariuki, kutoka Kenya manusura wa AMR, hatari hii si hadithi tu ni hali halisi kwani maambukizi aliyopata baada ya kufanyiwa upasuaji yalimweka kwenye hatari ya kupoteza maisha, baada ya dawa 17 kati ya 18 za viuavijasumu zilizojaribiwa kushindwa kukabiliana na maambukizi hayo. Ni nini hasa kilimtokea, na ana ujumbe gani kwa dunia katika wiki hii ya kuamasisha kuhusu usugu wa viuavijasumu?.
• Na nchini Zimbabwe, ufugaji wa samaki aina ya tilapia na matumizi ya teknolojia ya kidijitali vinawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata masoko mapya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, linasaidia uzalishaji wa vifaranga vya samaki, matumizi ya chakula mbadala chenye gharama nafuu na uuzaji wa bidhaa kupitia mitandao ya kijamii.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

