Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 NOVEMBA 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo inakupeleka Moyale eneo lililoko Kaunti ya Masarbit, kaskazini mwa Kenya ambako Assumpta Massoi kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP anatuelezea harakati za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakimbizi hao. Pia tunakuletea muhtasari wa habari. • Takriban watoto 64 wameuawa na wengine 64 wamejeruhiwa nchini Yemen tangu mapigano yalipozidi kushika kasi kuanzia mwezi Septemba mwaka huu, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF). Mapigano hayo yanayoendelea katika maeneo yenye wakazi wengi, hususan Taiz na Lahj, yanahatarisha maisha ya watoto na kuwanyima huduma muhimu. Msemaji wa UNICEF, Ricardo Peres ametoa wito akisema, pande zote zinazohusika katika mgogoro zinapaswa kuwalinda watoto na pia mashirika ya Kimataifa yanapaswa kuruhusiwa kuwafikia walio katika uhitaji mkubwa hivi sasa. • Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limewakutanisha huko Zanzibar, Tanzania, wataalamu wa afya na masuala ya fedha kutoka Afrika na washirika wa kimataifa. Mkutano huo wa siku tatu unalenga kuzisaidia nchi za Afrika kupata takwimu sahihi na za kina kuhusu kiasi cha fedha kinachowekezwa katika huduma hizo, jinsi fedha zinavyotumika na maeneo yanayohitaji uwekezaji zaidi. • Na leo imeanza Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics. Tayari takwimu za WHO zinaonesha kuwa Usugu wa mathalani bakteria dhidi ya dawa unahusishwa na vifo vya zaidi ya watu milioni 4.7 kila mwaka, na unaweza kusababisha vifo vya hadi watu milioni 39 ifikapo mwaka 2050. Mwenyeji wako ni Cynthia Akhangwa, karibu!
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.

