
JAMII INAKUJENGA AU INAKUPOTEZA? - MSASA NA MICHAEL KAMUKULU
Send us Fan Mail Tunakua tukiambiwa tusome, tupate kazi nzuri, tujenge maisha na tufanikiwe. Lakini kwenye safari hiyo, tunawahi kujiuliza kama tunachoendelea kukifukuzia kinaendana na sisi ni nani na kile tulichoumbiwa kufanya? Kila mmoja wetu ana uwezo fulani ndani yake. Lakini kuutambua uwezo huo, kuukuza na kuutumia kuleta thamani kwa wengine ni safari nyingine kabisa. Na safari hiyo inaathiriwa na mambo mengi zaidi ya tunavyofikiria. Kwenye episode hii ya MSASA, tumekaa na Michael na kuzungumza kuhusu namna familia, malezi, elimu na mifumo ya jamii inavyochangia kutujenga, kutuwekea mipaka au kutusaidia kufikia uwezo wetu. Ni mazungumzo yanayotufanya tujiulize maswali kuhusu namna tunavyoishi, tunavyopima mafanikio na nafasi yetu katika dunia inayotuzunguka. Je, unajua ulicho nacho ndani yako, na unakifanyia nini? Karibu MSASANI, tupate MSASA! ๐๏ธ Guest: Michael Host: Hisia MSASA PODCAST ๐๏ธ Website: https://neiked.co.tz/msasa/ Available on all major streaming platforms. #MSASAPodcast #Kujitambua #Uwezo #Elimu #Malezi #Jamii #Mitazamo #FikraTofauti
Audio and video play straight from the show's own hosting. PodSubs stores and serves no media.
